Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16  ya kutamba katika Bongo Fleva ya msanii JUMA NATURE maarufu kama Kiroboto pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi jumamosi hii ya tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala, kuanzia saa kumi na mbili jioni. 
 Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania. 
 Aidha, mashabiki watapata burudani kutoka kwa kiroboto ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao. 
 Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu. 
 Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya. 
 Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa kwetu sisi tunaamini Muziki unaongea.

 IMETOLEWA NA DENIS SSEBO, 
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM.
Mfalme wa Mchiriku Msaga Sumu akiongea. Kushoto ni msanii Snura na Kulia ni Meneja wa Mawasiliano na Mambo ya Sheria wa EFM Dennis Ssebo
Msanii wa kundi la Makomando akiongea akiwa na Snura na Msaga Sumu
Juma Nature, Snura na Makomando
Meneja mawasiliano na Mambo ya Sheria wa 93.7EFM Dennis Ssebo (mwenye suti) akiongea leo na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu onesho la hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi Jumamosi hii ya tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala. Kushoto na kulia ni wanaofanya kundi la Makomando, wakiwa na Snura (wa pili kushoto), Mfalme wa Mchiriku Msaga Sugu (wa tatu kushoto), Ssebo na Juma Nature.
Msanii JUMA NATURE a.k.a Kiroboto akiongelea onesho la hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi Jumamosi hii ya tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...