Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.

Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.

Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

“ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0062
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...