Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kimeshiriki maonesho ya 39 ya kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ili kuelezea umma juu ya shughuli zake mbalimbali ikiwemo masuala ya uendeshaji wa mikutano. AICC ilielezea pia uwepo wa kituo chake cha Mikutano kwa Mkoa wa Dar es Salaam kijulikanacho kama Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) chenye kumbi zenye uwezo wa kuhudumia wageni 10-1000. Mbali na masuala ya mikutano AICC pia iliweza kuwaelezea wadau mbalimbali waliotembelea banda lao juu ya huduma ya upangishaji wa nyumba za kisasa za makazi zilizopo eneo la Fire na Range Road jijini Arusha na uwepo wa nafasi za kupanga kwa ajili ya Ofisi kwenye Makao Makuu ya AICC.
 Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi Christopher C. Liundi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la AICC, kushoto ni Afisa Uhusiano na Itifaki Beatha Hyera na kulia ni Afisa Masoko na Utafiti Andes Seiya.
 Mwenyekiti wa Bodi ya AICC akibadilishana mawasiliano na mmoja wa wadau kutoka China alipotembelea banda la AICC

Afisa Masoko na Utafiti, Andes Seiya akiwaelezea wadau waliotembelea banda la AICC huduma zinazotolewa na AICC Picha  na Alfred Ngalaliji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...