Benki ya Exim  yajivunia  mafaniko maonyesho ya Saba saba.
USHIRIKI wa benki ya Exim kwenye maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam umeonyesha mafanikio makubwa ambapo pamoja na fursa nyingine benki hiyo pia imefanikiwa kusogeza huduma zake karibu kwa wateja wake wanaoshiriki na kuhudhuria maonyesho hayo.

Mbali na kutoa ushauri wa kibenki kwa washiriki na wateja wanaotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo, benki hiyo pia imeweka mashine ya ATM inayotembea jirani na banda hilo ili kuwapunguzia hadha ya kubeba kiasi kikubwa cha fedha wateja wake wanaofanya manunuzi kwenye maonyesho hayo sambamba na kujali usalama wa pesa zao.

Akizungumza na waandishi wa habari  kwenye maonyesho hayo mwishoni mwa juma lililopita, Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo, Bi. Agnes Kaganda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa weledi wa hali ya juu na maofisa wa benki hiyo wanaohakikisha  kila mteja anaetembelea banda hilo anaondoka  na uelewa wa kutosha kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo.

“Tumekuwa tukipokea wateja na wageni wengi sana wanaohitaji maelezo ya huduma zetu mbalimbali na kwa kweli pia tumefanikiwa kupata wateja wengi ambao wamefungua akaunti zao…kifupi washiriki wengi wameonyesha kuridhishwa na huduma zetu,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Bi. Kaganda mbali na huduma nyingine wateja wengi waliotembelea banda la benki hiyo wamekuwa wakipewa maelezo ya kutosha na faida kuhusu matumizi na usalama wa kadi za kutolea fedha za FAIDA zinazotolewa na benki hiyo.

“Pia tumekuwa tukiwahamasisha wateja na washiriki wanaotutembelea hapa kuhusu umuhimu wa wao kufungua akaunti ya amana (fixed deposit account)ambapo kwa sasa tunaendelea na kampeni ya kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni kuweka akiba,’’ alibainisha Bi. Kaganda.\
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Bi. Agnes Kaganda (wa kwanza kushoto) sambamba na mmoja wa maofisa wa benki hiyo wakitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo kwa mteja (aliyebeba mtoto) aliyetembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam-Saba saba mwishoni mwa juma lililopita.
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania (katikati)  wakifurahia moja ya zawadi kutoka benki hiyo walipotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam –Sabasaba. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo Bi. Elizabeth Mayengoh (wa kwanza kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...