Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema  kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. 
Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakaazi  wake hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika. 
Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...