Mchekeshaji maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi wiki hii.
Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.

Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000/- kupata burudani za muziki wa bendi na kwa wale watakaoingia kwenye disco la kukesha ni shilingi 20,000/-, na tiketi za V.I.P zitauzwa kwa shilingi 40,000/-.

“Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi” alisema Naamala.

Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Regency Park Hotel, Vibe Magazine, Bongo5.com, Michuzi Blog, Goethe Institut, Midundo Online Radio, CEFA, Timeticket, Nafasi Art Space, Eco Sanaa Arts Space, Creative Infinity, Kenya Airways, Apex Media, Iris Media, Kumkichwa Entertainment, Santuri Safari DJs na Legendary Music.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...