THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti
la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha
habari yenye kichwa cha habari, “Marais
watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.
Katika
habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia
nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara
mnono zaidi.
Gazeti
hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka,
ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.
Habari hizi siyo za
kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.
Mshahara
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata
wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.
Tangu
Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa
mishahara ya chini kabisa duniani.
Mshahara
wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa,
tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya
taasisi za umma nchini.
Aidha,
ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini,
linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya
nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.
Kwa
kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi
kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea
chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.
Ni
matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama
taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na
kuwaambia Watanzania ukweli.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Julai, 2015
Kwanini imeshindwa kuweka wazi Raisi analipwa kiasi gani kwa mwezi
ReplyDeleteSemeni. Basi kiiasi inashangza kwa hili mmejibu haraka sans. Toba
ReplyDeleteKuna shida ngapi za watanzania mbona ikulu hamjibu
Namkumbuka mwaka 2013, mtoto wa mkulima alituambia kwamba mshahara wake ni TSh milioni 7 kila mwezi; na kati na yeye na Makamo wa Rais na Rais - haizidi Miliono 1.. kwa hiyo nashangaa kusoma gazeti la kitaifa ikichapisha habari za kupotosha umma..
ReplyDeleteIla, ingekuwa vizuri pia.. in the spirit of full disclosure, ikulu nao wangetuambia mshahara halisi... hakuna kitu cha kuficha.. Kikwete ni mfano wa kuigwa tunapojadili mambo za Open Government!
sasa kama ni uongo si mseme huo mshahara? mnapofanya siri ndio mmaendekeza uvumi...kwa ninini siri?
ReplyDeleteMwananchi amekopi tu kama vilivyokopi vyombo vingine vya habari chanzo halisi cha habari hii kipo ktk lugha ya kingereza.Kanusho zuri ni lile lenye kuonesha uhalisia wa kiwango anacholipwa ili kuwaweka sawa watu haitoshi hata kusema eti tangu uhuru marais wa Tanzania ni miongoni mwa wanaopkea mshahara wa chini kabisa huku kiwango kikifichwa....kuweni wakweli kama HONOROUBLE JOCE MUJICA PRESIDENT OF URUGUAY dunia nzima zinamjua mtu huyu kwa uthubutu wake.
ReplyDeleteHuyu aliyekanusha taarifa hizi mbona ametumia mipasho badala ya kutumia fact figure reflecting reality to clear the atmosphere?????? hahahahaha ni kama ametumia nadharia kujibu swali la vitendo au kwa lugha nyepesi yenye kueleweka na wengi ni kwamba amebwabwaja badala ya kuelezea
ReplyDeleteILI KUZIMA KABISA UWONGO MKUBWA WA GAZETI HILO, NINGESHAURI KWAMBA, SERIKALI IPIGE PICHA " SALARY SLIP" YA MH. RAIS NA KUONYESHA HAPA KWENYE TAARIFA HII AU BASI SERIKALI ITAJE " EXACTLY" KIASI GANI MH. RAIS ANAPOKEA.
ReplyDeleteHAPO SERIKALI ITAKUWA IMEKATA KABISA SIO TU UWONGO HUU NA WONGO ZINGINE AMBAZO ZIMESEMWA WAKATI MWINGINE KUHUSU MH. RAIS.
Wajinga ndio watakaokubali kuwa raid analipwa mshahara mdogo kuliko watendaji wengine. Raid ndio anayepokea mahahara mkubwa kuliko MTU yeyote katika nchi take kwenye upande was serikali
ReplyDeleteMichuzi kwa heshima na taadhima naomba niseme haya yafuatayo : Huenda hiyo habari iliyoandikwa na gazeti la mwananchi inaweza kuwa ya kweli au siyo ya kweli ila kitu cha msingi hapa ni hawa watu wa ikulu kutoa taarifa na kisha kushindwa kuulezea umma kile ambacho wao wanakisema ni cha kweli.
ReplyDeleteKama walikuwa wanapingana na taarifa ya gazeti la mwananchi kwanini wao wasiseme mshahara halisi wa Rais wa JM Tanzania? watoe vigezo vyote halisi ili kuthibitisha tuhuma zao dhidi ya gazeti la mwananchi.
Au mshahara wa mtumishi wa umma, anayelipwa pesa na walipa kodi wa Tanznia ni siri ? !!
Nashangaa sana hawa watu wa habari wa ikulu wanaota taarifa ndefu lakini isiyo na vielelezo vyovyote. Au hiyo makala ya gazeti la mwananchi ina ukweli ndani yake ? !!
Tatizo liko wapi? si mtoe hizo figa!! tuambieni raisi wetu mshahara wake ni kiasi gani kwa mwaka? in dollars and shs. Vitu kama hivi vinahitaji UWAZI. Mbona mishahara ya waalimu tunaijua!!!!
ReplyDeleteLowassa is paying a lot of money to be a president!!! haiwezekani kukawa na mshahara mdogo. KUWENI WAWAZI
Kwa ufafanuzi tu, mshahara wa Rais wa Tanzania ni dola 190,000 tu, sio 192,000 kama African Review walivyozusha kwii kwiii kwiii.
ReplyDeleteKama Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilitaka Watanzania waambiwe ukweli kulikuwa na haja gani tena ya kulitaka gazeti la Mwananchi lianze kutafuta usahihi? Mambo mengine bwana...
Twambie TUNAMLIPA shilingi ngapi? Badala ya kuweka mlolongo wa maneno, ingekuwa vyema ukasema "Mheshimiwa Raisi halipwi $192K kwa mwaka, ila nalipwa $XXXK kwa mwaka." Hii ingefunga majadiliano na malumbano.
ReplyDeleteTaja basi analipwa shs ngapi? Mbona nimesoma habari yote hakuna sehemu inasema Raisi wa Tanzania analipwa shs ngapi. Tupeni taarifa wananchi ili tusisome habari za uongo.
ReplyDeleteWATANZANIA WENZANGU, MSHAHARA NI SIRI YA MTU, HAWEZI MTU YEYOTE KUTANGAZA MSHAHARA WAKE HADHARANI HATA SIKU MOJA, ILI IWEJE? HALAFU MKISHAJUA ANALIPWA SHILINGI NGAPI IWASAIDIE NINI? VITU VINGINE HAVIPASWI KUJADILIWA MITANDAONI, NA HUYO ALIYETOA SIRI ZA SERIKALI MITANDAONI ANATAKIWA ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU. MAANA NI KOSA KUBWA KUTOA SIRI ZA MTU MTANDAONI. AIDHA WAFANYAKAZI WA IKULU WAAPISHWE UPYA KAMA NI WAO NDO SOURCE OF INFORMATION. NARUDIA NDUGU ZANGU MTANIONA MPUUZI MSHAHARA NI SIRI YA MTU, SIRI KATI YA MWAJIRIWA NA MWAJIRI, RAIA MWINGINE HATAKIWI KUJUA MSHAHARA USIOMHUSU. .
ReplyDeleteHALAFU MSIWE NA MASHAKA MISHAHARA YA SERIKALI SI MIKUUUBWA KIASI HICHO MNACHODHANIA. KUWENI NA AMANI WAPENDWA. TUJADILI MAMBO YA MSINGI SIYO MSHAHARA WA RAIS.