Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa faragha wa mwaka cha makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na naibu makatibu wakuu mapema leo mjini Dodoma. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Nafasi na Wajibu wa Watendaji wa Wakuu wa Serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Kuingia Madarakani Serikali ya Awamu ya Tano.”
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Gallawa akizungumza kumkaribisha mkoani Dodoma Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala na Naibu Makatibu Wakuu wakati wa uzinduzi wa mkutano wa faragha unaouhusiana na watendaji hao wakuu wa serikalini unaoendelea katika ukumbi wa St. Gaspar leo mjini Dodoma. Mkutano huu wa siku mbili unatarajia kumalizika kesho.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa faragha wa mwaka cha makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na naibu makatibu wakuu mapema leo mjini Dodoma. Taasisi ya UONGOZI imeshiriki kama mwezeshaji wa mkutano huo, huku pia ikiwa imeandaa warsha mahusisi kwa ajili ya watendaji hao kuhusu masuala ya namna ya kuimarisha udhibiti wa ndani (Risk Management and Internal Control) serikalini.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (aliyeketi katikati), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Chiku Gallawa (aliyeketi watatu kutoka kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee (aliyeketi watatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja na makatibu wakuu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa faragha wa mwaka cha makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na naibu makatibu wakuu mapema leo mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...