Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa ya kifo cha Chifu wa Waluguru, Chifu Kingalu Mwanabanzi (pichani, enzi za uhai wake) ambacho kimetokea asubuhi ya leo, Jumatano, Julai Mosi, 2015 Kitengo cha Moyo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Dkt. Rajabu Lutengwe, Rais Kikwete amesema kuwa amepokea taarifa cha kifo cha Chifu Kingalu kwa mshtuko na majonzi.

  ”Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Chifu Kingalu ambaye nimejulishwa kuwa kilitokea asubuhi ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa hakika, kifo hiki kimeifanya jamii yetu kupoteza kiongozi aliyeendesha shughuli zake kwa busara kubwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Binafsi nilimjua Chifu Kingalu katika maisha yake. Alikuwa kiongozi mwenye busara na aliyetetea mila na tamaduni za watu wake. Alikuwa kiongozi mpenda watu na aliyejali sana maslahi na matakwa ya wafuasi wake. Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro salamu zangu za rambirambi nikikupa pole kwa kuondokewa na mmoja wa viongozi wa kijamii katika eneo lako.” 

“Aidha, kupitia kwako nawatumia wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro na wanajamii wa Kiluguru kwa kuondokewa na kiongozi wa tamaduni na mila zao. Vile vile, nakuomba unifikishie pole zangu nyingi kwa wanafamilia ambao wamepoteza mhimili wao. Naungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wangu. Naungana nao pia kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Chifu Kingalu Mwanabanzi. Amina.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Julai,2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2015

    R.IP...Dah nilimsoma huyu ktk historia kumbe alikuwepo bado ama kweli utandawazi si kitu yaani watu muhimu kama hawa hata uwepo wao hautambuliki tena hali ya kua wao ndio waliopelekea kuwepo taifa hili tulilonalo sasa. Usikute hata Kimweli,Mangi, Tiputipu meza na wengine...........

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2015

    Are we now back to having chiefs, mangis, sultans, wafalmes,etc.? I thought Mwalimu Nyerere helped us get out of this hereditary mess!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2015

    Do we still have chiefs, sultans, mangis, wafalmes, etc.? Didn't Mwalimu help us get out of this hereditary mess?!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2015

    Hiyo ni ceremonial post kwa sasa.

    Ni vyema ikawepo maana inasaidia kuweka discipline.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...