Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga akitoa taarifa ya Chama hicho kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa ndani ya Chama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa katika mkutano uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
 
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar.


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir/Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar   

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni Chama  kikubwa chenye wafuasi  na wanachama wengi  pamoja na  Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na uadilifu mkubwa.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga  wakati alipokuwa akitoa taarifa  kwa Waandishi wa Habari  kuhusu kujitoa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na Chama cha upinzani  huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui 

Amesema CCM ni Chama  kinacho aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa Tanzania  hivyo  kujitoa kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama haiwezi kukiathiri  chama hicho.

Nyawenga ameongeza kuwa wingi wa wanachama wa chama hicho  haujaletwa na utajiri wa vingozi wake bali umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi yake.

Alisema CCM haina hasara kumpoteza mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na itikadi ya Chama  kwa maslahi yake binafsi na marafiki zake hata kama utajiri  wake ni mkubwa wa kupindukia.

Ameongeza kuwa uwamuzi wa Lowassa kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la kukishituwa chama, viongozi, pamoja na wanachama wake na hakiwezi kudhoofika wala kutetereka.

Alisema hii sio mara ya kwanzi kwa Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi  mwandamizi  na kujiunga na  vyama vya upinzani na bado kinaendelea kuimarika.

“Mwaka 1989, CCM iliwafukuza uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino Lyatonga Mrema  na mwaka jana CCM ilimfukuza uanachama aliyekua Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,” alikumbusha Katibu wa Chama Mkoa.

Nyawenga aliweka wazi kuwa  umaarufu alionao  Lowassa inawezekana umejengwa kutokana na CCM lakini haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa kutokana na yeye.

Alisema wanachama wa Zanzibar  waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma  ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani ya Chama na sasa  baada ya kuhama wameamua kujitenga  na hawako pamoja naye.
 
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib Borafia Silima amesema kwamba Tanzania inaheshimika kuwa  ni  nchi yeye amani, na mshikamano na Chama cha Mapinduzi  kinafuata utaratibu wa katiba iliyowekwa.


Amesema kila Mwanachama anayo haki  na uhuru wa kuchaguwa kiongozi anayemtaka na yeye  kuchaguliwa na mtu yeyote ikiwa ni Demokrasia iliyotandikwa na Chama hicho.    

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...