Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo.
 Mmoja wa Wauguzi walioko kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU),akimpa maelezo mafupi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli alipokwenda kumjulia hali n kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wauguzi walioko katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa Mbeya,mara baada ya kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Meya Mama Kapinga mara baada ya kutoka kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.

 PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi kweli hizi siasa za Tanzania zikoje??? Magufuli anaruhusiwa kwenda kumjulia hali Meya aliyelazwa hospitalini lakini Lowasa akitaka kufanya hivyo, Polisi na NEC wanampiga marufuku eti anafanya kampeni nje ya ratiba????? Ndiyo maana wazungu wanatucheka na kutudharau kuwa watu weusi hawawezi kujitawala wenyewe kidemokrasia!!!.

    ReplyDelete
  2. Tangu lini kumjulia hali mgonjwa imekuwa siasa au kampeni! Hebu tufafanulie

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili ......unamtaka mdau wa kwanza akufafanulie wakati NEC ndio waliopiga marufuku kwa kutambua kwamba ina uhusiano na kampeni....we wa wapi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...