Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa
Sherehe za Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzes.
Muhubiri Mkuu wa Sherehe za Makambi mtaa wa Manzese Mch.
Idelphonce Tirumanywa akihutubia watu waliohudhuria sherehe hizo. Ujumbe Mkuu
"Mtizame Yesu Ukaishi".
Kikosi maalum cha vijana wadogo wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Manzese (Wavumbuzi) wakitembea kwa mwendo wa gwaride kuelekea jukwaani
kwa ajili ya program maalum kwenye sherehe za makambi.
Baaadhi ya washiriki wa sherehe za makambi wakisikiliza kwa
makini vipindi vinavyoendelea kwenye Makambi ya Mtaa wa Manzese.
Picha zote na Sarah Reuben.
SHEREHE za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa
kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea
Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo
mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa
kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na kanisa hilo. Mch.
Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la waadventista
wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema yatakayo warudisha
watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.
“Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa
sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato
wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi
nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.
Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka
Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa
huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...