Uongozi wa klabu ya Simba leo umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu iliyochezeshwa siku ya Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Zawadi zilizo kabidhiwa kwa washindi ni jezi pamoja simu, kila mshindi amepata jezi ya juu pea moja pamoja na simu moja aina ya Motec. Washindi wa zawadi hizo ni Jeremia Venist, Ahazi Mwembe pamoja na Marko Mgimba.
Mbali na zawadi hizo, klabu hiyo pia imekabidhi mipira nane kwa shule mbili za msingi za mkoa wa Dar es Salaam ambapo Shule ya Msingi Mikocheni A imepata mipira minne huku Shule ya Mingi Chang’ombe Mazoezi nayo ikikabidhiwa mipira minne.
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema, klabu hiyo inataka kusaidia soka la vijana nchini na kwasasa wameanza na mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae watasonga mbele hadi kwenye mikoa mingine ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa watoto ambapo ndio leno hasa la klabu hiyo kusaidia soka la vijana.

Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva  wa tatu kutoka kushoto akiwa na Washindi wa bahati nasibu  Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Iman Kajula (kulia)  na Msemaji wa Timu hiyo Haji Sunday Manara (kushoto).
Rais wa Simba Evans Aveva Akikabidhi Zawadi kwa Mmoja wa Washindi 
Washindi wa bahati nasibu  wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Rais wa Simba Evans Aveva akimkabidhi mpira mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...