Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo asubuhi.
Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Na Mwandishi wetu.
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
Vipindi hivyo
mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni
sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu
Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG),
Shirika la Kuendeleza Teknolojia za
Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na
kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za
vijijini na mijini.
Inakadiriwa kuwa mkaa
na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji,
wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012.
Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.
Kusoma zaidi bofya HAPA
Kusoma zaidi bofya HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...