SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limezindua rasmi kampeni yake
mpya inayojulikana kama “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kampeni ambayo ni endelevu inayolenga
kuboresha huduma ya Maji safi na salama maeneo yote ya jiji la Dar es salaam, pamoja na miji yote
ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, huku ikimhakikishia mwanamke kumpunguzia adha
ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi
Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni hiyo ina malengo ya kusogeza huduma ya Maji
karibu kwa kuhakikisha inaongeza wigo wa huduma ya Maji safi na salama kwa
kujenga vituo takribani 18 ambavyo vitakuwa vikitoa huduma ya Maji kwa wateja
wake kwa muda wa saa 24 kupitia wakala wake.
Katika
uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhandisi huyo pia alitoa rasmi kibali cha kuuza Maji
kwa watu wote wenye visima na magari makubwa (Maboza) huku akifanya usajili
bure kwa wauzaji hao wa Maji na wamiliki wa visima waliohudhuria uzinduzi wa
kampeni hizo, aliwataka wenye matanki kuacha kuchota Maji sehemu ambazo sio
rasmi kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha afya ya watumiaji wa huduma hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...