mwambene
Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) akionesha kitabu cha Katiba ya Tanzania kifungu kinachompa mamlaka Rais kufanya uteuzi ilikuboresha Serikali yake awapo madarakani. kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Vicent Tiganya. Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale.
DAR ES SALAAM Kufuatia vyombo vya habari nchini kuripoti taarifa kuhusiana na uteuzi wa Rais wa Wakuu wapya wa Wilaya uliofanyika hivi k aribuni, baadhi ya vyombo hivyo vya habari ikiwemo moja ya gazeti la kila siku nchini kuripoti kuwa uteuzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya kulipa fadhila na umetokana na masuala ya kisiasa na ni ufujaji wa wa fedha za umma. Hata hivyo Serikali imetolea ufafanuzi wa suala hilo kupitia Msemaji mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene amefafanua kuwa, Serikali imetimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu na Rais ana mamlaka ya kufanya uteuzi wakati wowote inapobidi kwa malengo ya kuboresha utendaji kazi Serikalini hivyo utezi huo wa Wakuu wa Wilaya ulizingatia vigezo vyote na taarifa hizo zilizoripotiwa na gazeti hilo ni za uzushi na za kupuuzwa.

“Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya uliofanywa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 4/10/2015 ambapo jumla ya Wakuu hao wapya wa Wilaya 13 waliteuliwa na wengine Saba kuhamishwa vituo vua kazi. 

Hii ni kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu alizonazo Rais” alieleza Assah Mwambene katika ufafanuzi wake kwa vyombo vya habari.
Na kuongeza kuwa, taarifa hizo zilizoripotiwa ni za kichochezi na zinalenga kumchonganisha Mhe.Rais na wananchi wake.

Mkurugenzi ihuyo, aliongeza kuwa, Serikali inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kufanya utafiti kwa kusoma nyaraka mbalimbali kuhusu mamlaka ya Rais na kujiridhisha kama uteuzi huo umezingatia matakwa ya Katiba ya nchi au la.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...