IMG_6069
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama wakipitia makabrasha ya mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema yaliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo (UNDP) kabla ya kuwasili mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
IMEELEZWA kuwa matatizo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hasa ya kutokuzingatiwa kwa sheria na kanuni za ushirika, wizi na ubadhirifu wa mali yamedhoofisha sana ushirika Mkoani Mwanza.

Hayo yamesema na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Mwanza.

Alisema kutokana na ukweli huo ni vyema vyama vya ushirika vikawa makini katika uchaguzi na kuhakikisha kwamba kila wanapofanya uchaguzi wanachagua viongozi wazuri wenye uchungu na maendeleo ya ushirika na siyo wanaotanguliza maslahi yao binafsi na kupuuza ya wengi.

“Tusaidiane kupambana na maovu na kujenga ushirika ulio imara.” Alisema.
Alisema pamoja na changamoto za kiuongozi Mwanza kwa sasa imepiga hatua kubwa upande wa SACCOS na VICOBA.
IMG_6523
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku moja juu ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa Wilaya yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
IMG_6528
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Ilemela, Manju Msambya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa nne kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Amon Manyama (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Mawasiliano wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa mradi wa Kukuza Uchumi, Kuleta Maendeleo Endelevu Kupitia Utunzaji Mazingira, Usawa wa Kijinsia na Kupunguza Mabadiliko ya Tabia Nchi, Margareth Nzuki (kushoto) katika picha ya pamoja na Wanawake Viongozi wa Vyama vya Akiba na Mikopo pamoja na Maafisa Ushirika wa Wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...