Kampuni ya Airtel Tanzania imeipiga
‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo
nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel
Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni yao inatambua mchango wa
waandishi wa habari za michezo nchini katika kuendeleza michezo na
kuamua kutoa vifaa vya michezo ambazo ni seti mbili za jezi na mipira.
Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada
huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.
“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa wa michezo na burudani, tumeshiriki
katika shughuli mbali mbali ikiwa kuendesha michezo ya Airtel Rising
Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi za timu ya waandishi wa habari za
michezo kuwakutanisha wana-habari na kushiriki katika mazoezi na mechi
kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na afya zao,” alisema Mmbando.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa
msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo. Majuto
alisema kuwa Taswa SC kwa kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa
vifaa hivyo na Airtel Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka
kutoa mchango wao.
“Tumeomba kwa kampuni nyingi, bado hatujapata majibu ya kukubaliwa au
la, Airtel Tanzania imeonyesha mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana,
ni faraja kwetu, tunawaomba wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.
Alisema kuwa Taswa SC bado inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine
kama viatu kwa timu zake za soka na netiboli na kuwaomba wadau
wafikirie kuwasaidia.
“ Tupo tayari kupokea vifaa vingine, timu
inatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira
ya mazoezi na mechi, hivyo kama kuna wadau wanataka kutusaidia,
wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza Majuto.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo moja wa wachezaji wa timu ya Taswa Queens , Imani Makongoro mara baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini. Akishuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary, baada ya Airtel kuchangia kwa vifaa hivyo kwa timu za mpira wa miguu na netiboli kwa timu za waandishi wa habari nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...