Mratibu wa Kampeni ya BINTI THAMANI wa Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania, Agnes Mgongo akizunumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO kuhusiana kampeni ya BINTI THAMANI itakayofanyika katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam na kampeni hiyo itakuwa inawalenga hasa wasichana ili kufikia malengo yao kwa kutumia fursa zinazotolewa na vyuo vya Don Bosco hapa nchini.
Mkurugenzi wa malezi ya vijana wa Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania, Padre, Dustan Haule akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa habari MAELEZO kuhusiana na harakati za kuwakomboa wasichana na uwepo wa kampeni ya BINTI THAMANI ambayo itafanyika katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam, pia amewakaribisha wadau na wafadhili mbalimbali katika kufanikisha kampeni ya BINTI THAMANI itakayo wawezesha wasichana ili kufikia maelengo na waweze kujitegemea katika jamii. Aidha alimtambulisha Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) pamoja na Mshereheshaji na Mchekeshaji MC, Pilipili kuwa watakuwepo katika kampni ya BINTI THAMANI  itakayofanyika Novemba 17 mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam. 

Kutoka kushoto ni Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) na Mshereheshaji na Mchekeshaji MC, Pilipili wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania leo katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) akizungumza na waandishi wa habari kuwa atatumbuiza katika kampeni ya BINTI THAMANI ambayo itafanyika Novemba 17 katika ukumbi wa King Solomoni  jinini Dar es Salaam. Pia aliwasihi wasichana kujitokeza kwa wingi ili waweze kuwahamasisha wasichana wengi zaidi ili kujipatia mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza waandaaji wa kampeni ya BINTI THAMANI itakayofanyika Novemba 17 mwaka  katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...