Uongozi wa maandalizi ya  onesho la mitindo ya mavazi la kila mwaka la "Lady In Red 2016" umekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa "Danken House" jijini Dar es salaam kujadili na kutoa hamasa kwa Designers na wadau mbalimbalia ambao ni wapenzi wa mitindo.

Uongozi huo ambao unasimamiwa na Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin  umesema kuwa "Jukwaa la "Lady In Red 2016" litakuwa la ainayake kufuatia jitihada na juhudi zinazofanywa na walengwa wa tukio hilo, ambalo linategemea kupandisha Designers wengi zaidi hapa nchini siku ya Jumapili 31/1/2016 katika ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni kwa Warioba  jijini Dar es salaam.

Miongoni kati ya Designers watakao panda kwenye Stage siku hiyo ni Bemy Masai, Kelly Peter, Faustin Simon, Mtetesi Forcus, Barnabas, Mwanahamis Kiroho, Nelson Thomas, Walter Demarian, Dorine Lymo, Evemary Sospeter, Fatma Rashid, Samweli Zebedayo, Kulwa Mkwandule, Jocktan Makeke, Saleem Siwila, Love Delamo, Abdul Mwene, Karol Mngumbi Jay Julius, Furaha, Joshua, Benja, Lili, Veronica, Rukia Walele nk.

Hivyo kama wewe ni mpenzi wa mitindo usikubali kupitwa na tukio hilo, kiingilio ni buku 10000/= na viti vya mbele ni 30000/= Nyote mnakaribishwa ulisema oungozi wa maandalizi ya Tukio hilo.
DSCN9613
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin  akiongelea mambo yatayopamba Jukwaa la Lady In Red 2016
DSCN9625
Mbunifu wa mitindo wa kimataifa Martin Kadinda akifafanua jambo.
DSCN9650
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akitambulisha safu ya designers wataoshiriki katika onesho hilo la kukata na shoka
  DSCN9657   Picha za Pamoja za Designers mara baada ya kumaliza mazungumzo ya "Lady In Red 2016" na waandishi wa Habari leo,​(Picha na Maelezo by Victor Petro from Super News Tz)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...