Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi (pichani kulia) , ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia. Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa, huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer akipata 7.86%. Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd (pichani kushoto) , ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayechezea Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa mataji matano msimu uliopita. Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...