Herieth Paul mwanamitindo wa Kitanzania anayeishi jijini New York, Marekani ambako anafanyia kazi zake ameingia mkataba na kampuni ya vipodozi ya kimataifa ya MAYBELLINE ya New York, Marekani na kutangazwa kuwa BALOZI wake wa kimataifa  kuanzia mwezi Februari 2016; shughuli ambazo zitamfanya kwenda maeneo mbalimbali yakiwemo Bara la Ulaya, Marekani, Afrika, Asia na kwingineko duniani. Kampuni ya Maybelline ilimtangaza rasmi hivi karibuni, Mwanamitindo wa Kimataifa Herieth Paul, akiwa ni Mtanzania wa kwanza Mwanamitindo kuunyakua ushindi huu mkubwa.

 Herieth mwenye umri wa miaka 20 aligundulika kuwa na kipaji hicho akiwa na umri wa miaka kumi na nne (14) akiwa nchini Canada alipokuwa akisoma na kuishi na wazazi wake.

Mbali na uteuzi wa kuwa BALOZI wa kampuni ya Vipodozi ya Maybelline, Herieth Paul amefanikiwa kufanya kazi na makampuni mbalimbali ya mitindo na vipodozi duniani ikiwepo kampuni ya Diane Von Furstenberg, Lacoste, Tom Ford, Zac Posen, Phillip Lim, Mac, Sephora nk...,

Mwanamitindo wa Kimataifa Herieth Paul ambaye ameipeperusha Bendera ya Tanzania Dunia nzima anafanya masomo yake ya Chuo kwa njia ya mtandao na pia akijihusisha na shughuli za kijamii nyumbani alikozaliwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watoto yatima na wale wenye mazingira magumu  ili waweze kutimiza malengo yao ya kimaisha ikiwa ni pamoja na elimu na mahitaji yao ya kila siku.

Mafanikio ya Herieth ni mfano wa kuigwa na vijana wa Kitanzania kwa kuwa na uamuzi sahihi, malengo dhabiti na bidii ya kazi, ni vichocheo muhimu vinavyoweza kufanya mtu afanikiwe katika maisha. 
Gazeti la GLAMOUR la New York, Marekani lilifanya mahojiano na Bi Herieth Paul wakati wa sherehe fupi ya kuteuliwa kwake iliyofanyika jijiji New York Marekani:

Lipstick:     Hongera kwa kuteuliwa kuwa Balozi wa Maybelline na kuwa mmoja kati ya wasichana waliokwisha kufanya kazi na kampuni hii. Je, kati ya wasichana waliowahi kufanya kazi na Maybelline ni nani anayekuhamasisha sana?.

Herieth:    Sijui niseme ni nani kati ya Christy Turlington na Jourdan Dunn. Christy ni mwanamke mwenye bidii ya kazi, ni mzazi na anasaidia mashirika yanayohudumia wasiojiweza. Jourdan pia ni mzazi na anatoa misaada kwa watu wengine.
       
Lipstick:    Ni mwanamke gani anayekuvutia sana kwa urembo?

Herieth:    Mama yangu, ana uzuri wa asili, ngozi ya mwili ambayo ni nyeupe kidogo kuliko yangu ambayo inameremeta. Lakini pia anampenda Beyoncé.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...