NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya Habari

HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti cha rais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.

Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne usiku.
Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutoka New York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.

Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo.
Clinton ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...