Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Mwaka 2015 Serikali ya Tanzania ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na kuanzisha mafunzo kwa kada mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community Health Workers). Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii huduma za afya za msingi.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MPANGO  mkakati  wa Sekta ya Afya  wa  Mwaka 2016 /2017 unahitaji sh.trioni 21 katika kuweza kutekeleza maeneo nane  ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na wadau wa afya leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali itahakikisha inakwenda sambasamba na mpango huo  kutokana na kugusa kila sehemu ikiwa ni lengo la kumfikia mwananchi wa kuweza kupata huduma ya afya.

Amesema eneo mojawapo ni utoaji wa kinga ya afya kwa jamii pamoja na elimu juu ya magonjwa kwa kuweka wataalam wenye mafunzo kutoka sehemu husika.
Ummy amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 4000 ambao watafanya kazi na jamii moja kwa moja katika utoaji wa kinga ya afya pamoja na elimu juu ya magonjwa mbalimbali.
Amesema katika eneo la pili ni mgawanyo wa rasilimali fedha kwa kuhakikisha kila kituo kinapata fedha na takwimu zake zitahifadhiwa juu ya fedha wanazozipata kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.

Waziri, Ummy, amesema katika eneo la tatu ni juu ya uchangiaji wa huduma ya afya bado ni changamoto hivyo katika mpango wanatarajia kupeleka mswaada bungeni kwa kuwa na mfuko  moja ambao kila mwananchi atachangia kwa ajili ya huduma ya afya.

Aidha amesema katika mpango huo wataangalia watumishi wa sekta ya afya kuwa kila sehemu wanakuwepo katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo pamoja na masilahi ya motisha kwa watumishi walio pembezoni.

Waziri Ummy amesema katika eneo lingine katika mkakati huo ni kuweka ufumbuzi wa wa upatikanaji fedha na vyanzo vyake vikaeleka na uendeshaji pamoja na rasilimali watu wanapatikana.
Amesema sehemu ya nane ni utoaji wa nyota  katika vituo vya afya ambavyo vitapimwa kutokana na utoaji wake kwa kuanzia nyota ya kwanza hadi ya nne.

Mkuruegenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria amesema hayo mambo yalikuwa yakisubiliwa kwa muda mrefu na sasa serikali imeamua kuwajibika katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wake.

Amesema kuwa mpango mkakati ukienda kama ulivyopangwa jamii ya kitanzania itaweza kupata huduma bora ya afya kutokana na mikakati iliyomo katika mpango huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...