Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wmwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko"unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sija base kwenye khabari husika, ispokuwa namshkuru sana Rais wetu wa awamu ya tano Mh. JP Magufuli. Maana hapo tena ingekuwa ni 'isirafu' tupu ya manywaji na makulaji kufurutu ada, kisa na mkasa ati kuna kikao/mkutano, thubutu! Kwenye himaya ya mzee wa "HapaKaziTu" Hivyo hivyo vichupa vya maji vinakidhi haja in case mtu kapaliwa na sauti au ana kiu, tena vinapendeza Masha Allah vikipangwa mezani kama hivyo, maana vyote muonekano wake ni 'uniform'. Hopeful kwa mwendo huo huenda tutajaaliwa kufika mahali ambapo Tanzania ya leo inapotaka iwe, in all aspects. In Sha Allah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...