Mwanamuziki nyota nchini Vanessa Mdee, akiweka dole gumba tayari kuchapa kwenye fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati wa kongamano lililowakusanya wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule ya Biashara na kufanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki. Mamia ya wanachuo walijiunga na mpango huo baada ya kupata elimu ya faida za kujiunga na mpango huo. Wanaoshuhudia, kutoka kulia ni Balozi wa PSPF, Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS wa Mfuko huo, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko na Uhusiano wa PSPF, Rahma Ngassa.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akizungumza kwenye kongamano la wanafunzi wanawake wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Shule ya Biashara), chuoni hapo. Kushoto ni Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanya kazi zake Ulaya na Marekani, Flaviana Matata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...