JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa likielekea kiwanda cha Saruji cha Tanga.
Rais Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

"Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo" alisema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, na amewapa pole majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.
Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.

11 Februari, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nikisikia simbamtoto nachoka kabisa! liliua kaka yangu likamtumbukiza wami na mkwe wetu ambaye ni mkwe wa kaka yangu aliyetumbukizwa wami. Namuimagine wifi yangu akiliona hilo basi ama akisikia habari za ajali za hili basi inakuaje maana kwake ni baba na mume wake vifo vyao vimesababishwa na Simbamtoto katika matukio tofauti.

    ReplyDelete
  2. Jamani hizi ajali za barabarni kwa Tanzania zitawamaliza watu kwa uzembe wa madereva.Imefika wakati sasa kwa viongozi wa ngazi za juu kabisa kulikemea na kulizungumzia suala hili.

    ReplyDelete
  3. Tunaungana na Rais wetu kutuma rambirambi zetu. Pamojana hayo kuna misemo isemayo ukimuona mwenzako ananyolewa wewe tia maji.

    Jana jhapamaeneno ya Ferry kuendea Kigamboni tuliona tukio ambalo labda halijawafikia na kulisia kwa wakubwa nchini. Kulitokea ajali ya kivuko cha Pantoni. Ilikuwa almanusura watu wapoteze maisha. Mungu hakupenda hivyo nasi tunamshukuru. Naomba kwa heshima na taadhima wewe binafsi Mheshimiwa Rais tilia maanani suala hili la kivuko cha Kigamboni. Ni suala nyeti na tusipokuwa makini tutapoteza roho zawapendwa wetu. Tulikuona Mheshimiwa Rais kabla hujawa Rais wakati huo ukiwa na Waziri mwenye dhamana ya hapo Kigamboni ulikuwa mstari wa mbele na mara kadhaa tulikutana na wewe hapo ukifanya ukaguzi. Tafadhali ninakuomba kwa heshma na taadhima tupiamacho kivuko hicho ni hatari sana. Huu ni ushauri wangu tu binafsi. Nakutakia kazi njema wewe Mheshimiwa Rais pamoja na watendaji wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...