Hali ya simanzi yaukumba mkoa wa Geita baada ya radi kuua watu 3 wa familia moja kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.https://youtu.be/xCc2OKhSG9k
Uongozi wa Mgodi wa Tanzanite One ulioko Mererani wawafukuza wafanyakazi 201 kwa tuhuma za kufanya mgomo usio halali na kuharibu miundombinu. https://youtu.be/cxX13rhIA1Y
Zaidi ya mifugo 200 wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakatwakatwa mapanga na wakulima wakiwatuhumu wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba yao. https://youtu.be/pCEZ-MAnjLQ
Shule ya msingi Majengo iliyoko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma yaelezwa kutokuwa na huduma ya choo tangu kuanzishwa kwake. https://youtu.be/xAmiu2PbrpY
Idara ya mahakama nchini yajipanga kuanza ujenzi wa mahakama katika ngazi 4 ikiwemo mahakama za mwanzo, wilaya, mkazi na mahakama kuu baada ya kupokea shilingi bilioni 12 kutoka serikalini. https://youtu.be/at6dBSY84Y8
Serikali yasema ipo katika mchakato wa kuboresha shirika la ndege Tanzania ATC ili liweze kufanya kazi kibiashara;https://youtu.be/OqeXaIR5M7Q
Serikali yasema itaunda upya kikosi cha kulinda wanyapori ili kupambana vilivyo na suala la ujangili nchini;https://youtu.be/_LqK_RQ279k
Serikali yasema inaanza kuangalia ujuzi unaotolewa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kama unachangia maendeleo ya wananchi pamoja na kukuza uelewa miongoni mwa wanafunzi husika;https://youtu.be/sNtvDrVhv6s
Wazee katika kambi ya Kalwande mkoani Mwanza waiomba serikali iwasaidie msaada wa chakula; https://youtu.be/Hgaq7-ML944
Jeshi la polisi visiwani Zanzibar lapiga marufuku vitendo vya kusamba vipeperushi vyenye ujumbe wa vitisho;https://youtu.be/QbddFe9Qo10
Mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kukamilika mwezi Juni mwaka huu;https://youtu.be/d9tmm8pPLGw
Mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Jakaya Kikwete aahidi kuendeleza upanuzi na uboreshaji wa chuo hicho;https://youtu.be/M9rnBG3TnkU
Wabunge wa mkoa wa Kigoma wameunda umoja wa kushughulikia mipango ya maendeleo kwa ajili ya mkoa huo;https://youtu.be/fG2D3ldrvPw
Serikali imebuni na kutekeleza sera ya kumuwezesha mwananchi kiuchumi ili mwananchi aweze kufaidika na rasimali zilipo nchini;https://youtu.be/XeSmBQEUwFw
Serikali yawataka wafanyabiashara nchini kulipa kodi zao kikamilifu ili kuiwezesha serikali kutimiza ahadi yake ya kuwahudumia wananchi; https://youtu.be/-Pknr0z76M8
Timu ya Yanga inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Mauritius kwa ajili ya mchezo wake wa ligi ya mabingwa dhidi ya timu ya Cercle de Joachim; https://youtu.be/_YzshddYyDc
Inaelezwa watu wasiojulikana katika mkoa wa kusini visiwani Zanzibar wazichora alama ya X nyumba zipatazo 31 zinazosadikiwa kuwa ni za wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM;https://youtu.be/9A8H2xKiDZg
Serikali wilayani Magharibi visiwani Zanzibar yasitisha ujenzi wa kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Mtoni;https://youtu.be/3MQvVHF3oaA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...