Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Wema wa siku tatu wa watafiti kutoka nchi za Afrika wa kutathimini utendaji kazi wa Wema kwa mwaka uliopitaKushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uharishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Dk. Denis Kyetere na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Ushirikiano Mradi wa Wema, Kampuni ya Monsanto, Mark Edge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Programu, Taasisi ya Bill and Melinda Gates Dk.Lawrence Kent (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kampuni la kimataifa la Monsanto na mbegu za GM (Genitically Modified)lazima watafiti wawe makini maana Tanzania ikikubali tu mbegu za GM basi mbegu zote zitakuwa zinatoka kampuni ya Monsato na usalama wa hifadhi wa cahkula na mbegu zitakuwa mikononi mwa mashirika ya nje ya Tanzania.

    Tuendelee kutumia mbegu zetu toka vituo vya utafiti vya Ukiluguru n.k kwa manufaa ya usalama wa kuzalisha na kuhifadhi mbegu na nafaka bila kuwekwa rehani nje ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...