Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.


KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 

Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni kwa Mnyamani.

Uharibifu huo uligundulika leo asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo ikielekea stesheni ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.

Tayari mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho kama kawaida.

Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,



Nd Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Februari 09, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...