Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande wamekutana kwa ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na uendeshaji wa kesi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyon itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.

Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa ambayo hazina mahakama kuu.

Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili wananchi waweze kupata haki.

Amesema hatua za ujenzi wa Mahakama ya Wahujumu Uchumi na Wala Rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya mahakama.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3 zitakazotumika  katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu Serikali kuendelea kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ili kuwezesha ufanisi wa shughuli zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sawa ila zitumike kwenye malengo kusudiwa musizichakachue

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...