Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pongezi za dhati na za pekee kwa Mh. Rais wetu JPM kwa uteuzi wake mpya wa wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara. Pia pongezi za dhati na za pekee pia kwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda, kwa kweli utendaji wake umekuwa ukionekana siku hadi siku, kwa kweli anastahili ukuu huo wa Mkoa na hata zaidi ya hapo. Kwa kweli amekuwa na moyo wa dhati wa kujituma na kuwa karibu sana na wananchi wake katika suala zima la maendeleo ya Wilaya yake aliyokuwa akiitumikia awali kabla ya uteuzi huo mpya. Naamini pia na wote walioteuliwa na Mh. Rais JPM katika uteuzi huu wa Wakuu wapya wa Mikoa, watakwenda sambamba na kasi yake mpya aliyoanza nayo kwa kuzingatia awamu ya tano siyo ya lelemama bali ni wito wa 'HapaKaziTu' kwa vitendo na siyo bla bla tena. Mungu Ibariki Tanzania na Raia wake wote, Ibariki Afrika na dunia kwa jumla.

    ReplyDelete
  2. Hapa kazi
    Pongezi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa uteuzi wa wakuu wa mikoa Tunaimaini watakwenda na Kasi ya Rais John Pombe Magufuli napenda pia kutoa pongezi sana kwa Rais kwa kumteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wenye mikiki mingi Yuko Vizuri kijana hatuna wasiwasi naye ni mchapa kazi na anakwenda na kasi ya Rais Mungu ibariki Tanzania.

    Tunamuomba Mungu Ampe afya njema, Rais wetu John Pombe Magufuli amlinde katika kazi zake za kila siku tunaimani mapaji saba ya Roho mtakatifu yako ndani yake Hekima, Akili, Shauri, Nguvu, Elimu, Ibada na Uchaji wa Mungu. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...