Kampuni ya wino na vifaa vingine vinavyotumika katika uchapaji ya Cartridge World yenye makao yake makuu Hong Kong nchini China imezindua duka la vifaa hivyo jijini Dar es Salaam lengo likiwa kusaidia kupunguza gharama za uchapaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World, Rajesh Pandya alisema kuanzishwa kwa duka hilo nchini kutasaidia kupunguza gharama za uchapaji kwani wino na vifaa vingine vya uchapaji vya kampuni hiyo sasa vitapatikana kwa bei nafuu.

Alibainisha kuwa kampuni hiyo itakuwa pia inatengeneza vifaa hivyo nchini vikiwa katika ubora unaoitambulisha kampun I hiyo ulimwenguni ambako ina matawi katika nchi 50 ulimwenguni na maduka zaidi ya 700 Marekani na 130 nchini Uingereza.

Alisema unafuu wa bei utawezesha kushuka pia kwa gharama za uchapaji na hivyo kuwapa nafuu wahitaji wa huduma za uchapaji na pia katika kuliepusha Taifa na uharibifu wa mazingira, kampuni hiyo itakusanya vifaa vilivyotumika hususan vya kuhifadhia wino na kuviteketeza.

Alisema duka litrakuwa na matawi katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza kwa kuanzia na wigo zaidi utapanuliwa ili kutosheleza mahitakji ya huduma za Catrtridge nchini.

“Kifaa cha kuhifadhi wino katia mashine ya uchapaji kikitupwa ardhini kinaweza kuchukua hata miaka 400 hadi kuharibika hivyo kampuni yetu ulimwenguni kote inakusanya vifaa hivyo vilivyotumika na kuziunda upya kabla ya kuviingiza tena sokoni lengo likiwa kuepusha uharibifu wa mazingira” alisema.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mandeleo ya biashara Kimataifa, Harry Stoubos alisema kufunguliwa kwa duka hilo nchini ni njia ya kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Tanzania ndio nchi pekee ukanda wa Afrika Mashariki ambako duka linafunguliwa.

“Tanzania ndio nchi ya kwanza Afrika Mashariki na tunatarajia kupanua wigo zaidi katika ukandaa huu ili tuwe na martawi katia nchi zote za Afrika Mashariki” alisema na kuongeza kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ndio ambayo imewavutia kuwekeza nchini.
Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni ya Cartridge,Harry Stoubos (kushoto), akimkabidhi kabrasha Mkurugenzi Mtendaji wa Catridge World-Africa Mashariki, Rajesh Pandya ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka la vifaa kuhifadhia wino katika mashine za uchapaji vya kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World kwa Africa Mashariki, Rajesh Pandya na Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo,Harry Stoubos wakionyesha kwa waandishi wa habari vifaa vya kuhifadhia wino katika mashine za uchapaji wakati wa uzinduzi wa duka hilo, jijini Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...