Na Avila Kakingo , Globu ya Jamii.
 KITABU cha HOW TANZANIA CAN MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi (akimwakilisha waziri mkuu Kassimu Majaliwa), Kitabu hicho kimetungwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hisani ya Ofisi ya waziri mkuu.

akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa
kitabu hicho kicholenga kwenye mada  ya  "Tanzania Move from Poverty to Prosperity", hasa kwa kipindi hiki, ikizingatiwa kwamba Serikali ya awamu ya tano ipo katika vita ya kupambana na adui umaskini ili tuweze kufikia malengo ya millennia ya mwaka 2025. 

 "Chapisho hili la kitabu (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) limetolewa wakati sahihi kwa taifa letu Tanzaniani chapisho la aina yake toka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam linaloonesha kiu ya wataalamu, wanataaluma na wale wanaotekeleza Sera  kutaka taifa letu lijikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini na kufikia ustawi katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, na kisiasa." Amesema Dkt. Possi.

Kwa upande wa Mhadhir wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally amesema kuwa dhima ya kitabu cha  (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) inalenga uchumi wa watu kwa watu wenyewe.

Pia amesema kuwa kitabu hicho kimegusia suala la maliasili na umhimu wake kwenye mageuzi wa uchumi wa viwanda Tanzania, uvuvi, madini, misitu kilimo na nguvu kazi ya gharama nafuu pia kimetaja umhimu wa Diplomasia ya kiuchumi, mifumo ya kitaifa ya Sayansi na tecknologia, ubunifu usalama wa raia na mali zao. 
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kilichotungwa na wahadhili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu hicho kimezinduliwa katika ofisi za waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo akiwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam..
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akiwa na baadhi ya wahadhiri, watunzi wa kitabu na waalikwa wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa  kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii. 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...