Na Bashir Yakub.
Marehemu atakapokuwa ameacha shauri mahakamani ambalo alikuwa anashtakiwa nalo kabla ya kufa kwake basi hukumu itakapotoka itatakiwa kutekelezwa. Hapa tunaongelea hukumu itokanayo na mashauri ya madai. Sambamba na hilo makala yataangalia pia mambo kadhaa yanayohusu kifo cha mtu ambaye alikuwa akishitakiwa/akilalamikiwa mahakamani kabla ya kifo chake. Amri ya xxii kanuni ya 1 – 12 ya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai ndiyo itakayotuongoza.
1.JE MSHITAKIWA AKIFA NA KESI ITAKUFA.
Kanuni za jumla (general rule) ni kwamba shauri hutakiwa kufunguliwa na mtu aliye hai dhidi/akimshitaki mtu aliyehai. Hii ni kanuni ya jumla yenye kumaanisha kuwa mtu aliyekufa hawezi kushtaki wala kushtakiwa. Hata hivyo kwenye kanuni za sheria pale penye kanuni ya jumla( general rule) huwa kuna vinginevyo( exception). Hii ina maana yapo mazingira ambapo mshitakiwa atakufa lakini kesi yake haitakufa itaendelea.
2. KESI KUENDELEA HATA BAADA YA KIFO CHA MSHITAKIWA/MLALAMIKIWA.
Ikiwa marehemu alikuwa ameshtakiwa/amelalamikiwa katika kesi ambazo zinahusu mali kama nyumba, gari, kiwanja na mali nyinginezo na akafa kabla ya kesi hiyo kuisha basi kesi hiyo itaendela. Pia ikiwa alishitakiwa katika mashtaka yanayohusu masuala ya mikataba pia kesi hiyo nayo itaendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...