JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI  YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA




        

TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa mwaka 2015/2016.
Taarifa hizo zinazosambazwa zinaeleza kwamba walimu wapatao 17,928 wa cheti (Daraja IIIA) , 5,416 wa Stashahada kwa sekondari na 12,677  kwa  shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara wamepangwa kwa ajili ya kuanza kazi.
Katika taarifa hiyo inawataka walimu hao waliopangwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi tarehe 01/04/2016.
Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa walimu ambao hawataripoti ifikapo tarehe 10/04/2016 hawatapokelewa tena na watakuwa wamepoteza ajira zao.
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa hizo kuwa ni za upotoshaji. Wananchi wanapaswa kuzipuuzia kwani mpaka sasa bado Serikali haijatoa ajira za walimu kwa mwaka 2015/2016.
Ajira mpya za ualimu zitakapokuwa tayari zitatangazwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari na katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
Imetolewa na :
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
11/03/2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...