Idhaa ya Kiswahili ya DW imeanzisha huduma mpya: Mukhtasari wa habari ndani ya sekunde 100. Mbali na kukuletea matangazo ya redio ya kila siku kwa ajili ya Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu, Jumatatu hadi Ijumaa DW itakupatia video fupi zenye habari. 
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt, ana furaha kwamba yeye na timu yake ya waandishi wa habari kutoka nchi tano tofauti wanaanzisha huduma hii mpya itakayoitwa Papo kwa Papo na itakayokuwa jicho la kuutazama ulimwengu. 
Kupitia video zetu utaweza kupata habari muhimu za kimataifa za kila siku.
“Papo kwa Papo” itapatikana katika chaneli ya YouTube ya DW Kiswahili, Facebook na toleo fupi la sekunde 60 litarushwa kupitia WhatsApp.
Miongoni mwa mambo mengine, tutakuletea “hashtag” zilizovuma pamoja na katuni za kisiasa kutoka kwa wasanii maarufu Gado na Said Michael.
Pamoja na hayo, kila Ijumaa DW Kiswahili itakuletea sekunde 100 za matukio muhimu ya kisiasa yaliyotokea katika juma zima.
·         Tafadhali kuwa shabiki wetu YouTube: www.youtube.com/kiswahili
·         Jiunge nasi katika ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/dw.kiswahili.
·         Pata “Papo kwa Papo” na taarifa zaidi kupitia WhatsApp. 
Unaweza kujiunga nasi kupitia kiungo hiki: bit.ly/1Q86kjt 
Kila siku Idhaa ya Kiswahili ya DW inarusha masaa matatu ya matangazo Afrika Mashariki na katika eneo la Maziwa Makuu. Kwa kushirikiana na redio washirika katika eneo zima, DW inawapatia wasikilizaji habari zisizoegemea upande wowote kuhusu yanayojiri duniani kwa ujumla na hasa barani Afrika kupitia masafa ya FM. Ili kutoa mtazamo huu wa kimataifa, timu ya waandshi wa habari kutoka nchi tano inafanya kazi na mtandao mkubwa wa waandishi walioko Afrika na kwengineko.
Matangazo ya Kiswahili ni miongoni mwa matangazo ya DW yenye wasikilizaji wengi zaidi. DW inajumuisha vipindi vilivyopokea tuzo kama vile Learning by Ear - Noa bongo, jenga maisha yako - na vipindi vinavyojadili afya, haki za binadamu, mazingira, wanawake na maendeleo, vijana na utamaduni na sanaa. 
www.dw.com/kiswahili
Waliosimama kutoka kushoto Daniel Gakuba, Iddi Ssessanga, Grace Kabogo, Sudi Mnette, Bruce Amani na alieketi Caro Robi
Kuangalia video clic link ifuatayo: 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...