Shujaa Wetu, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.

Alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi (Climate Change) ambapo alihutubia Ƶakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana duniani.

Kutoka Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.

"Kitu ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa balozi wao". Alisema Getrude.
"Wazazi wawaruhusu watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi ili waweze kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao". Anasema Mtoto Mwanahabari Getrude.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. You made all of us proud Getrude we heard you, we encourage you to do your best in school, do no put away your confidence, you are destined to good things in this country and beyond.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...