Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kuongezwa kwa safari moja ya ziada kwa kila awamu ya usafiri huo kuanzia siku ya Jumatatu Aprili 25, 2016. Hivyo basi awamu ya asubuhi na ile ya jioni itakuwa na safari 4 badala ya 3 za sasa, halikadhalika muda wa kuanza safari nao umebadilishwa. 
Kwa awamu ya asubuhi treni ya kwanza itaondoka Ubungo Maziwa kuja kituo kikuu cha Dar es Salaam saa 12:15 ambapo itawasili saa 12:55. Safari ya mwisho ya nne itaondoka Ubungo Maziwa saa 5:15 asubuhi kwenda Kituo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Kwa awamu ya jioni kutoka Kituo Kikuu cha treni cha Dar es Salaam safari ya kwanza itaanza saa 10:00 jioni  itawasili Ubungo Maziwa saa 10:40 jioni. Safari ya pili kutoka Kituo cha Dar es Salaam itaanza saa 11:40 na kuwasili Ubungo  Maziwa saa 12:20 jioni. Halikadhalika safari ya 3 itaanza kutoka kituo cha Dar es Salaam saa 01:20 usiku na ile ya 4 saa 3:00 usiku kwenda Ubungo Maziwa. 
Halikadhalika taarifa hii ya mabadiliko ya safari za treni ya jiji imeainisha kuwa Kituo cha Kamata kitatumika kwa safari zote 4 za awamu ya jioni kwenda Ubungo Maziwa  na kurudi Kituo cha Dar es Salaam.
Uamuzi huu umechukuliwa ili kukidhi maombi ya abiria waliokuwa wanataka kituo cha Kamata kitumike kwa huduma ya treni ya Jiji awamu ya jioni.
Aidha wito maalum umetolewa na Uongozi wa TRL kuwa abiria na wadau wote wa huduma ya treni ya Jiji kufuata kwa makini maelekezo ya wahudumu wa treni hiyo ili kuongezwa kwa safari za huduma hiyo kuwe na tija kwa abiria na Kampuni ya TRL.

RATIBA MPYA YA TRENI YA JIJI KUANZIA APRILI 25, 2016


AWAMU     YA ASUBUHI
KITUO
KUWASILI
KUONDOKA


UBUNGO MAZIWA
SAA 12:05
SAA 12:15


DAR
SAA `12:55
SAA 01:05


UBUNGO MAZIWA
SAA 01:45
SAA 01:55


DAR
SAA 02:35
SAA 02:45


UBUNGO MAZIWA
SAA 03:25
SAA 03:35


DAR
SAA 04:15
SAA 04:25


UBUNGO MAZIWA
SAA 05:05
SAA 05:15


DAR
SAA 05:55


AWAMU YA JIONI





DAR

SAA 10:00


UBUNGO MAZIWA
SAA 10:40
SAA 10:50


DAR
SAA 11: 30                                                     
SAA 11:40


UBUNGO MAZIWA
SAA 12:20
SAA 12:30


DAR
SAA 01:10
SAA 01:20


UBUNGO MAZIWA
SAA 02:00
SAA 02:10


DAR
SAA 02:50
SAA 03:00


UBUNGO MAZIWA
SAA 03:40
SAA 03:50


DAR
SAA 04:30



Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Aprili 22, 2016.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...