Muda mfupi uliopita Mapunda ameimbia mbeyacityfc.com kwamba kwa kosa hilo City ilistahili kupata ushindi huo wa bao 3 na pointi 3 kama ambavyo kanuni za ligi zinavyoelekeza na kutoa angalizo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kuongeza umakini katika kutunza kumbukumbu za adhabu au makosa mbalimbali kwa wachezaji wake.
“Kwenye hili nalipongeza shirikisho, hakika wametenda haki, na ninawaomba waendelee kusimama kwenye misingi ya haki, ni haki yetu kupata pointi 3 baada ya Azam fc kuchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kadi 3 ambaye ni wazi hakustahili kucheza mchezo ule, hata sisi tumekutana na hali hii katika nyakati tofauti lakini hatukuwahi kuthubutu kumchezesha mchezaji mwenye adhabu hata kama alikuwa ni muhimu kikosini” alisema.
Akiendelea zaidi Mwenyekiti Mapunda alisisitiza vilabu kuwa makini na matukio ya aina hii huku pia akiikumbusha TFF kuendele kuchukua hatua kama hizi.

Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa bado anaamini TFF itaitendea haki City kwa kuchukua hatua kama hizi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliovunjika dakika mwisho za kipindi cha pili baada ya kutokea kwa vurugu kubwa uwanjani zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo ya Tanga.

“Naamini TFF watatutendea haki kwenye hili pia,mchezo ule ulikuwa na matukio mengi ya ajabu ambayo yalimfanya mwamuzi kushindwa kumaliza mchezo, risasi za moto zilipigwa uwanjani, , sisi bado tunasubiri pointi tatu zingine kutoka kwenye mchezo ule, kwa sababu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”, alimaliza.
Mwenyekiti wa Mbeya City fc, Mussa Mapunda amelipongeza shirikisho la soka Tanzania TFF kwa hatua yake ya kuipoka pointi 3 timu ya Azam Fc na kuziweka kwa timu yake kufutia makosa yaliyofanywa na timu hiyo ya Chamazi Complex kumchezesha mchezaji Erasto Nyoni aliyekuwa na zuio la kadi tatu za njano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...