Waendesha pikipiki zipakiazo abiria jijini Dar (Bodaboda) usiku huu wamefunga Barabara ya Mandela eneo la Riverside, Ubungo kwa kupanga mawe na kuegesha pikipiki zao, baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari ambayo ilitoweka eneo la tukio. Wamedai kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo wa kafunga Barabara hiyo, kwa kuwa wamekuwa wakidharauliwa na watu wenye magari, hivyo wamechukua uamuzi huo kushinikiza na wao kuheshimiwa kama vyombo zingine vya usafiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2016

    Nchi ya WAGARATIA NANI ALIWALONGA? Kila mtu anashika sheria mikononi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2016

    Dawa kuwapiga chini maeneo ya mjini. Ndumu, viroba na vyombo vya usafiri wapi na wapi???!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2016

    Ujinga kama huu ukiruhusiwa kuendelea ama kuvumiliwa ndio hufanya nchi zisitawalike. Break down ya law and order kwenye nchi inaaanza kidogo kidogo. Waulize Kenya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2016

    Kuendelea kuwalea bodaboda kwa sababu zozote zile kutakuja kuleta maafa makubwa siku zijazo, kwani tabia ya kuhisi kudharauliwa iko kwa kila mtu ajionaye dhaifu kwa mwingine, hata madereva wa magari madogo hujiona vivyo hivyo kwa wale wa magari makubwa au mabasi na wa mabasi hujiona hivyo hivyo kwa wale wa malori makubwa, lakini hujawahi kuona akigongwa ajionaye dhaifu wengine wenye vyombo kama chake wakiamua kuchukua sheria mkononi. hii himaya ya muungano usio rasmi wa watu wa aina fulani wenye kujimilikisha maamuzi ya kisheria dhidi ya wengine ikiachwa iendelee itazaa kundi ambalo linaweza kuwa hasi, si kwa wengine tu, bali hata kwa serikali na vyombo vyake vya dola, ni muhimu na ni lazima nguvu ya ziada itumike kuzuia na kukomesha kabisa mawazo haya, kwani tunajiundia bomu lisubirilo kulipuka kwa kishindo na kusababisha maafa yasiyokifani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...