Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa FNB Tanzania, Silvest Arumasi (katikati) akiwa na Meneja Masoko wa benki hiyo Blandina Mwachanga (kulia) na Meneja Mauzo wa benki hiyo, Moise Rajabu (kushoto) wakizindua kampeni mpya ya benki hiyo kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba benki ili waweze kuwekeza na kuwa na kujikimu wakati wa dharula katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
 Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kimtandao na Bidhaa wa FNB Tanzania, Silvest Arumasi (katikati) na pamoja na Meneja Mauzo wa benki hiyo, Moise Rajabu (kushoto) na Meneja Masoko wa benki hiyo Blandina Mwachanga (kulia) wakizindua kampeni mpya ya benki hiyo kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba benki ili waweze kuwekeza na kuwa na kujikimu wakati wa dharula katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. 

Benki ya FNB Tanzania imezindua kampeni mpya ya kuweka akiba ijulikanayo kwa jina la million a month award (Mama) ili kuwatunuku wateja waliopo na wapya ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuhamasisha Watanzania kuweka akiba kwa ajili ya mustakabali salama wa kifedha. Mkuu wa Huduma za Digitali wa FNB, Silvest Arumasi alisema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba shilingi milioni kumi zitatolewa kila mwezi kwa washindi kumi ambapo jumla ya shilingi milioni 30 zitatolewa kwa wateja katika muda wa miezi mitatu kuanzia Juni mwaka huu.

 Arumasi alisema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo itakayochukua miezi mitatu kwamba kwamba wateja wapya na waliopo watapata nafasi ya moja kwa moja kushiriki kwenye droo kutokana na kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao na kuweza kujishindia zawadi kila mwezi kwa miezi mitatu ya kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki. “Kila mwezi tutafanya droo moja na kuchagua washindi kumi kati ya wateja wetu ambapo washindi hao kumi na kila mmoja atajipatia zawadi ya shilingi milioni moja”. 

 Arumasi alisema kampeni hii inafungua milango ya fursa kwa Watanzania kujiwekea akiba kwa faida ya badae na inawapa fursa ya kusimamia vizuri matumizi ya fedha zao na hatimaye kuwa na utamaduni wa kuweka akiba huku wakizidi kujijengea nidhamu katika mapato na matumizi “Kupitia kampeni hii tunataka kuhimiza utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa wateja wetu ili waweze kuwekeza na kuwa na msaada wakati wa dharula. Hii ni njia mojawapo ya kujenga jamii imara yenye uhakika wa kuishi maisha bora,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...