Na Dr. Hamisi Kigangwalla

Huyu binti anaitwa Getrude Clement. Anatokea Jiji la Mwanza, nchini Tanzania. Alipata fursa ya kipekee kuongea kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa, akikaribishwa na Mhe. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama muwakilishi wa watoto na vijana wote duniani. Ana umri wa miaka kumi na sita. 

Jana alikaribishwa kuongea kwenye kikao cha wabunge watetezi wa haki za watoto, alitoa hotuba iliyowatoa watu machozi. Baba yake ni kinyozi na mama yake ni mfanyabiashara mdogo mdogo wa nyanya na vitunguu, na yeye anasoma kidato cha tatu, shule ya sekondari Mnarani (shule ya sekondari ya kata). 

Kwa kuthamini kipaji chake na mchango wake, na kutambua nafasi yangu kama Naibu Waziri kwenye Wizara inayosimamia mambo ya Watoto, na kama Mbunge na Mzazi wa mabinti, lakini zaidi kama mtu kutoka kwenye background ya maisha ya chini na ninayethamini mchango wa elimu kwenye maisha yangu, nimeamua kujitolea kumsomesha kidato cha tano na cha sita kwenye shule za kisasa. Taasisi yangu ya misaada ya kijamii ya Hamisi Kigwangalla Development Foundation itamlipia ada za masomo yake ya high school.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2016

    Huu ni mchango mzuri katika maisha ya Getrude. Wazazi endelea kudunduliza msaidie maendeleo ya vijana wenu. Wanaokuwa kwenye shida wakiinukia wanafika mbali wakiwa na mchango mkubwa katika jamii kwa sababu ya kukumbuka walikotoka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2016

    Msaada mkubwa! Hongera sana!

    Lau kama kila mtoto wa Kitanzania angeweza kuingia hizo 'shule za kisasa' bila kipingamizi kutokana na umasikini; tuondoe kabisa kukuza apartheid katika mfumo wa elimu!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Getrude Clement kwa uwakilishi wako mzuri, pia Ubarikiwe sana Mh. Waziri Kingwangala kwa kuuona na kuuthamini mchango wa pekee wa mtoto Getrude Clement ambae alijaaliwa kupata fursa ya pekee ya kuongea kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa akiwa kama muwakilishi wa watooto na vijana wote duniani. Hii ni fakhari iliyoje kwa nchi yetu ya Tanzania. Umefanya la maana kujitolea kumsaidia Getrude kwani tayari kipaji chake, ari na kiu ya kusonga mbele vimejidhihirisha wazi. Naamini kina Getrude wapo wengi, lakini mfano wako Mh. Kingwangala, utasisimuwa ari hata kwa wengine kuwa na moyo huo wa kuwainuwa na kuwasaidia khusuan kitaaluma mabinti wengi ambao ni mithli ya Getrude kwa namna moja ama nyingine, ili kujenga Taifa imara la kesho litakalokuwa na mabinti wengi wasomi na wenye vipaji kwa manufaa ya nchi yetu kwa jumla.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2016

    Nachukua fursa hii kukupongeza Mheshimiwa Kigwangallah kwa moyo huu na ni muelekeko mzuri kwa wale wenye uwezo wa kusaidia wengine.Ni jambo lisilofichika kuwa kuna wenye nacho na wasio nacho katika jamii zetu na tangu Enzi zote zilizowahi kuwepo hapa duniani, Sitaki kuwa na muelekeo hasi bali tuwe na muelekeo chanya. Wale wote wenye uwezo, huu ni muongozo mzuri. Mungu akubariki Mheshimiwa Kigwangallah. Kutoa ni moyo usambe si utajiri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...