Katika pita pita za hapa na pale, Kamera ya Globu ya Jamii ilifanikiwa kuzinasa baadhi ya taswira kadhaa katika Barabara ya Morogoro rodi jijini Dar es salaam hasa katika ile njia maalum kwa mabasi ya endayo haraka. 

Njia hii imekuwa ikipendwa sana kutumiwa na ndugu zetu waendesha Bodaboda, kwa madai kwamba hiyo ni njia nyepesi zaidi kwao kwa safari zao. Lakini njia hiyo si yao na wanafahamu fika matumizi ya njia hiyo, lakini bado wao wanaendelea kujiachia tu, kana kwamba hawafahamu lolote au ni njia iliyotengenezwa kwa matumizi yao. 

Ni hivi karibuni Mabasi hayo yaendayo haraka yameanza kufanyiwa majaribio katika njia hizo, ila cha kushangaza kama si chakustaajabisha ni pale ndugu zetu hao wa Bodaboda wanapoendelea na matumizi ya njia hiyo, na wakati mwingine kulazimisha kutaka kulipita hata basi hilo katika sehemu ambayo hata ujiti hauwezi kupita. 

Jambo hili yapaswa kuangaliwa kwa jicho kali sana, maana kama vijipu upele hivi vitaendelea kuwepo, basi kuna siku vitakuja kuwa vidonda vikubwa na vishindwe kutibika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2016

    Wakikamatwa wanadai wanaonewa. Tuache kuwapa kiburi lazima wafuate sheria.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2016

    Wasimazi wa sharia wako legelege... Kuvunja sharia sio kuonewa bali ni utukutu. Bila ya kuwapa adhabu wanajenga kiburi na kukaidi hadi wachapwe viboko... (Samaki mkunje angali mbichi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...