Na Bashir Yakub.
1.WAKFU NININI.
Sheria ya Mirathi na
Usimamizi Mali Sura ya 352 ndiyo sheria
inayoeleza masuala yote ya msingi
kuhusu habari nzima ya Wakfu.
Kwa mujibu wa
sheria hiyo kifungu cha 140 Wakfu ni
kutoa mali kulingana na sheria
za kiislam kwa ajili ya dini, hisani au
kwa ajili ya watu/mtu wa familia fulani.
Suala la Wakfu huenda sambamba na suala la wadhamini.
Kwa mujibu wa kifungu hicho wadhamini ni watu/mtu ambaye
ndiye hupewa jukumu la kusimamia mali ya wakfu.
Kama ni nyumba yenye wapangaji basi
mtu au watu hao ambao ni wadhamini ndio watahusika
na kukusanya kodi pamoja na mambo mengine yote yanayohusu
nyumba.
Na kama kuna maendelezo yoyote ya
ukarabati au vinginevyo hawa ndio watahusika.
2. MAELEKEZO
YA MTOA WAKFU LAZIMA YAFUATWE.
Siku zote mtoa wakfu hutoa mali kwa malengo maalum.
Yaweza kuwa malengo ya kiimani au vinginevyo.
Mtoa wakfu anapotoa nyumba/kiwanja kama wakfu
hutoa kwa maelekezo ya namna na jinsi kitakavyotumika.
Kwa namna mtoa wakfu atakavyotoa maelekezo ndivyo hivyo
inavyotakiwa kuwa.
Ni kosa mali ya wakfu kutumika kinyume na maagizo ya mtoa wakfu.
Ikiwa itatumika kinyume basi kuwe na sababu za msingi
ambazo zinalazimisha hivyo.
Ziwe ni sababu ambazo
hakuna namna isipokuwa ni lazima
kufanyika hivyo. Kifungu cha 150
( 1 )
cha sheria ya mirathi na usimamizi wa mali kinasema kuwa matumizi ya mali za wakfu ni lazima yazingatie nia na malengo ya mtoa wakfu.
Isipokuwa kifungu hicho kinasisitiza kuwa nia na malengo ya mtoa wakfu yatafuatwa tu pale ambapo nia na malengo hayo yatakuwa halali kisheria.
Ikiwa mtoa wakfu ameelekeza matumizi ambayo hayakubaliki kisheria basi maelekezo hayo
hayatafuatwa. Lakini
ikiwa hayapingani na sheria yoyote basi ni sharti kuyafuata.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...