Jengo la NSSF la eneo la Akiba jijini Dar es Salaam jioni hii limeshika moto ambao kwa bahati nzuri Jeshi la Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio na kuudhibiti.  Chanzo cha moto huo kinasemekana ni kulipuka kwa mtungi wa gesi katika moja ya vyumba vya ghorofa ya juu katika jengo hilo liitwalo Akiba House.
Magari ya Jeshi la Zimamoto yakiwa eneo la tukio katika harakayi za kupambana na moto huo katika jengo la NSSF  lililopo eneo la Akiba jijini Dar es Salaam muda huu. Moto huo inasemekana hakuna madhara makubwa (ya kibinadamu) yaliyojitokeza baada ya Jeshi la Zimamoto kufika kwa wakati katika eneo hilo. Picha na Prince Ali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...