Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, leo wamekutana kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania- TCAA, Banana- Ukonga, jumla kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro.Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCAA, Bwana Mbwana J. Mbwana na wajumbe wengine wa bodi hiyo, Prof. Arnold J. Temu, Hanif M. Malik. Yussuf M. Ali, Jaffari K. Mpili na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza S. Johari .

TCAA yenye jukumu la kisheria la kusimamia na kudhibiti masuala ya ki- usalama, kiuchumi katika sekta ya usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege, hutoa leseni kwa kampuni zinazoomba kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini baada ya kampuni hizo kukidhi vigezo na kanuni zinazosimamia sekta.

Mikutano hiyo ya kupitia maombi ya leseni za usafiri wa anga hufanyika kila mwaka ambapo maombi ya kampuni mpya na zile ambazo tayari zinafanya shughuli zake hupitiwa na wadau na kujadiliwa , kabla ya bodi ya wakurugenzi wa bodi kuridhia na kutoa leseni kwa kamapuni husika.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania( TCAA) Mbwana J. Mbwana(wapili kushoto) akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari.(kushoto)  wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro,Wengine kutokkulia ni wajumbe wa Bodi  Hanif M. Malik na Jaffari K. Mpili. 
 Badhi ya wadau wa usafiri wa anga Tanzania wakiwa kwenye  mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea  na wadau mbalimbaliwakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)  Mbwana J. Mbwana(wapili kushto) akiongoza kikao hicho .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...