Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na wanachi wa maeneo ya Manzese, wakati akitoa wito wa kuwataka wanaojifunza mambo ya kivita katika sehemu za ibada kuacha mara moja, kwani hiyo si kazi yao na wala hailipi. Kamanda Sirro aliingia mtaani kutoa somo hilo kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuendeleza jitihada za kuimarisha ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.
Kamanda Sirro akiendelea kutoa somo kwa wamazi wa maeneo ya Manzese, Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wananchi walioitikia wito wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, alipokuwa akitoa somo kuimarisha ulinzi na Usalama Jijini. Mkutano huo ilifanyika kwenye viwanja vya Manzese jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...