KING DREW 404 AAGWA NA WATANZANIA KUTOKA KILA KONA ZA MAREKANI HAIJAWAHI KUTOKEA.

Hapa ni mzazi mwenzie Andrew na mtoto wao mpendwa Zoe wakiwa mbele ya mwili wa marehemu.Mwili wa marehemu utawasiri Dar_Es_Salaam siku ya jumanne na jumatano asubuhi ndugu na jamaa wa Dar_Es_Salaam watafanya Ibada ya misa na kuaga mwili ndani ya kanisa la Lutheran nyuma ya Ubungo Plaza kisha safari ya Dodoma jioni na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis May 05.

Mwakilishi wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani angeongea mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa na kuaga mwili wa Andrew.

Mtoto wa Marehemu akiwa mbele ya mwili wa baba yake uku akiwa ameshikiliwa na Wash rafiki wa marehemu kutoka Ohio. Kwa Taswira zaidi ya kila kilichokuwa kimendelea siku hiyo ya Tar. 30 nenda soma zaidi.

Mzazi mwenza wa marehemu Emmy akitoa neno mbele ya watu waliojitokeza kuaga mwili wa baba wa mtoto wake.

Michael Nyanda kutoka Maryland rafiki wa marehemu akitoa machozi mbele ya mwili. 

Wash kutoka Ohio akiwa na majonzi mbele ya mwili wa marehemu 

Majonzi kwa kila mmoja aliepita mbele ya mwili marehemu.

Wengine walishidwa hata kuangalia sura ya marehemu kwani ilikuwa ni ngumu kuamini.

Ny Ebra kutoka New York nae ni mmoja kati ya watu waliotoka nje ya Houston, TX hapa akipata ukodak na Emmy mzazi mwenza wa marehemu na mtoto wao Zoe. 

Mzazi mwenza wa marehemu Emmy Matafu pamoja na mtoto wake Zoe katikati. Picha kwa hisani ya Vijimamboblog. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2016

    What's up with these dark glasses in-doors😎!?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2016

    There are different kinds of shades,some can be won indoors if not all...some are ultraviolet screen for out doors..ok my dear?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...