Na David Mwaipopo, Globu ya Jamii

Kuelekea michuano ya kabumbu ya Kombe la Amerika ya Kusini (Copa America), Globu ya Jamii itakuwa inawaletea taarifa kwa ufupi juu ya michuano hiyo maarufu na ya kusisimua ambayo itaanza kutimua vumbi Ijumaa Juni 03, 2016 nchini Marekani.

Kwa ufupi leo tunaangazia ni kwanini michuano hii inafanyika ikiwa ni takribani mwaka mmoja tu baaada ya ile iliyotangulia ya Mwaka 2015 badala ya kusubiri miaka mine kama ilivyo kawaida ya michuano hii, pia kwanini mwaka huu inafanyika nchini Marekani?.

Michuano hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1916 nchini Argentina na kushirikisha mataifa manne ambayo ni Uruguay, Brazil, Argentina na Chile. Hivyo mwaka huu inatimiza miaka 100 na ndiyo sababu kubwa ya kufanyika michuano hii.
Marekani huwa ni nchi mualikwa katika michuano hii, lakini mwaka huu wamepewa heshima ya kuandaa michuano hii kwa sababu ya kutotoa upendeleo wowote kwa moja ya nchi mwanachama wa shirikisho la kabumbu la Amerika ya Kusini kuweza kuandaa michuano hii mikongwe kabisa duniani.

Kesho katika simulizi hii tutawaletea idadi ya timu shiriki na wasifu wa timu hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2016

    Taarifa inasema michuano hivyo ''itaanza kutimua vumbi'' tarehe 3 Mei 2016?!! Na hii leo ni Mei 31, 2016

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...